Monday, November 29, 2010

Wikileaks yafichua siri za Marekani


Julian Assange
Mjumbe mmoja wa baraza la Congress amependekeza Wikileaks iorodheshwe kama kundi la kigaidi
Tovuti ya Wikileaks, maarufu kwa kutetea sera za uwazi, imeanza kuchapisha mawasiliano ya siri kati ya balozi za Marekani kuhusu viongozi wakuu duniani.
Baadhi ya mawasiliano yaliochapishwa ni yale kati ya Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia na Marekani, pale alipopendekeza vikali kuwa Iran ishambuliwe kijeshi.
Serikali ya Marekani imekashifu hatua hiyo ya kuchapisha mawasiliano hayo. Imesema kuwa kitendo hicho kinahatarisha maisha na mabalozi wake.
Lakini mwanzilishi wa tovuti ya Wikileaks Jullian Assange, anasema serikali ya Marekani haitaki kuwajibishwa.
Wikileaks imechapisha nakala mia mbili kati ya zaidi ya laki mbili ilizonazo ya mawasiliano hayo. Hata hivyo nyaraka zote hizo zimesambazwa kwa magazeti kama vile New York Times la Marekani na The Guardian la Uingereza.
Masuala yalioangaziwa zaidi kwenye mawasiliano hayo ni mpango wa nuklia wa Iran, ufisadi katika serikali ya Afghanistan na uhusiano kati ya serikali ya Urusi na genge la mafia.
Amri ya waziri wa mambo ya nje wa marekani Hilary Clinton kuwa vigogo wa Umoja wa Mataifa akiwemo katibu mkuu achunguzwe pia imechapishwa.

Saturday, November 27, 2010

Wasio wavutaji hufa kwa kuvuta sigara

Utafiti mpya uliofanywa na shirika la afya duniani WHO unaonyesha kuwa watu 600,00 wasio wavutaji sigara hufariki kila mwaka kutokana na kuvuta moshi unotokana na kukaa karibu na watu wanaovuta sigara.
Mvutaji
Mvutaji sigara

Utafiti huo uliochapishwa siku ya Ijumaa ndio wa kwanza duniani kuangazia hasa madhara ya moshi wa sigara.
Shirika la WHO lilichukua takwimu kutoka karibu kila taifa duniani. Takriban asilimia 40 ya watoto na zaidi ya asilimia 30 ya watu wazima ambao hawavuti sigara huwa wanakabiliana na moshi kutoka kwa wavuta sigara.

Kulingana na utafiti huo watu 600,000 hufariki kila mwaka thuluthi yake wakiwa watoto.
Sigara
Wasio vuta huatrhirika pia

Moshi unaowafikia watu ambao hawavuti sigara unaweza kusababisha maradhi ya moyo, pumu na hata saratani ya mapafu kama tu inavyofanya kwa wavuta sigara.
Tofauti hata hivyo ni kwamba wale wanaofikiwa na huo moshi hawafanyi hivyo kwa uamuzi wao wa kuhatarisha afya yao kwa kutumia tumbaku.
Hofu kubwa kulingana na waliochapisha ripoti hiyo ni athari kwa watoto hata katika mataifa ambayo yana sheria kali dhidi ya uvutaji sigara kwa sababu bado wanaathirika kutokana na watu wanaovuta nyumbani.
Ingawaje ni vigumu kuunda sheria kubana watu kuvuta sigara nyumbani, WHO inakiri kuwa kuna haja ya hatua kuchukuliwa ili kulinda watoto kutokana na madhara ya moshi wa sigara.

Wednesday, November 24, 2010

MCHEZAJI BORA WA BBC WA MWAKA 2010

Wachezaji
Wanaowania tuzo
Bofya Bofya hapa kupiga kura:
Pata kwa undani na maoni ya wataalam kuhusu wachezaji watano nyota kutoka Afrika wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC kutoka Afrika.Wacheza hao ni Asomoah Gyan, Didier Drogba, Yaya Toure, Samuel ETO'O na Andre Ayew vijana wanaotisha kwasa huko Ughaibuni.

Kikwete atangaza baraza la mawaziri

Mwisho wa habari !!

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza lake jipya la mawaziri kukamilisha uundaji wa serikali tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Dr Jakaya Kikwete
Kikwete amewaacha mawaziri kadhaa wa zamani na kuteua sura mpya kama vile Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Kikwete alitaja serikali yake mbele ya waandishi wa habari katika shughuli iliyofanyika Ikulu mjini Dar Es Salaam, akibainisha kuwa hakuna mabadiliko makubwa katika idadi ya wizara, zipo jumla ya wizara 26.
Sura mpya kadhaa zimetajwa ikiwa ni pamoja na Profesa Anna Tibaijuka atakayesimamia wizara ya ardhi na makazi.Profesa Tibaijuka alikuwa mkurugunzi mkuu wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa kabla ya kujiuzulu na kwenda kugombania ubunge jimbo la Muleba Kusini.
Waziri aliyetajwa kinyume na maelezo ya wachambuzi wengi wa kisiasa ni Samuel Sitta, baada ya kuondolewa kiti cha spika wa bunge la Muungano, sasa anakuwa Waziri wa maswala ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wengi wa serikali iliyopitwa wamerejeshwa tena katika majukumu waliyokuwa nayo awali kama vile Bernard Membe atakayeendelea kusimamia mambo ya nje.Mustapha Mkullo anarudi kuongoza wizara ya fedha.
Marekebisho kadhaa ameyataja Rais Kikwete katika uundaji wa baraza lake kuwa idara ya vijana imeondolewa kutoka wizara ya kazi na kuhamishiwa wizara ya habari na michezo.
Wanasiasa kadhaa waliokuwa katika serikali iliyopita wameachwa, baadhi yao ni wasomi maarufu kama Profesa Peter Msola aliyekuwa Sayansi na Teknolojia, Profesa Juma Kapuya aliyekuwa Kazi na Profesa David Mwakyusa aliyekuwa afya, mwingine ni kada wa chama kama John Chiligati aliyeachwa wizara ya ardhi.
Waziri hao wataapishwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Ikulu ya Dar Es Salaam.
Orodha kamili ya mawaziri na manaibu waziri hii hapa chini.

Namba

Ofisi/Wizara

Waziri

Naibu Waziri
1. Ofisi ya Rais 1. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Utawala Bora
Mathias Chikawe
2. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
3.
Ofisi ya Makamu wa Rais
1. Muungano
Samia Suluhu
2. Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa

4.
Ofisi ya Waziri Mkuu
1. Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi
2.Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu

5.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
George Mkuchika 1.Aggrey Mwanri
2. Kassim Majaliwa
6.
Wizara ya Fedha

Mustapha Mkulo 1. Gregory Teu
2. Pereira Ame Silima
7.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Shamsi Vuai Nahodha Khamis Kagasheki
8.
Wizara ya Katiba na Sheria
Celina Kombani
9.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard Membe Mahadhi Juma Mahadhi
10.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dr. Hussein Mwinyi
11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo Benedict Ole Nangoro
12.
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa Charles Kitwanga
13.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna Tibaijuka Goodluck Ole Madeye
14.
Wizara ya Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige
15.
Wizara ya Nishati na Madini
William Ngeleja Adam Kigoma Malima
16.
Wizara ya Ujenzi
Dr. John Magufuli Dr. Harrison Mwakyembe
17.
Wizara ya Uchukuzi



Omari Nundu Athumani Mfutakamba
18.
Wizara ya Viwanda na Biashara
Dr. Cyril Chami Lazaro Nyalandu
19.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru Kawambwa Philipo Mulugo
20.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Haji Hussein Mpanda Dr. Lucy Nkya
21.
Wizara ya Kazi na Ajira
Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
22.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Sophia Simba Umi Ali Mwalimu
23.
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo
Emmanuel Nchimbi Dr. Fenella Mukangara
24.
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Samuel Sitta Dr. Abdallah Juma Abdallah
25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe Christopher Chiza
26. Wizara ya Maji Prof. Mark Mwandosya
Eng. Gerson Lwinge

Tuesday, November 16, 2010

Mwana Mfalme William kuoa

Mwana mfalme William atafunga ndoa na Kate Middleton mwaka ujao, kwa mujibu wa taarifa kutoka jumba la kifalme jijini London, Clarence House.
William
Kate Middleton na Mwana Mfalme William
William, ambaye ni mrithi wa pili wa kiti cha ufalme, atafunga ndoa mwakani, katika mwaka ambao ungeadhimisha miaka 30 ya ndoa ya wazazi wake.
Wawili hao waliweka ahadi ya uchumba mwezi Oktoba nchini Kenya, wakati wakiwa katika mapumziko.
Kate
William na Kate kufunga ndoa
William na Kate walianza kuwa na mahusiano miaka minane iliyopita, wakati wakisoma katika chuo kikuu cha cha Mtakatifu Andrews huko Fife, ambapo pia waliishi katika nyumba moja.
Ndoa hiyo imetangazwa katika taarifa fupi iliyotolewa na Clarence House.

Taarifa

Taarifa hiyo imesema: "Mwana Mfalme wa Wales, ana furaha ya kutangaza ndoa ya mwanae, Mwana Mfalme William atakayofunga na Bi Catherine Middleton.
"Harusi itafanyika wakati wa majira ya joto ya mwaka 2011, mjini London. Taarifa zaidi kuhusu harusi hiyo zitatangazwa baadaye.
"Mwana Mfalme William amemfahamisha Malkia na ndugu wengine wa karibu.
Kate
Kate na William
"Mwana Mfalme William pia ameomba ruhusa kutoka kwa baba wa Bi Kate.
"Baada ya kufunga ndoa, wawili hao wataishi kaskazini mwa Wales, ambapo Mwana Mfalme William ataendelea na kazi katika jeshi la Anga la Uingereza Royal

His Excellence President Jakaya Kikwete when addressing the Parliament on 21.8.2008