Mwana mfalme William atafunga ndoa na Kate Middleton mwaka ujao, kwa mujibu wa taarifa kutoka jumba la kifalme jijini London, Clarence House.
Wawili hao waliweka ahadi ya uchumba mwezi Oktoba nchini Kenya, wakati wakiwa katika mapumziko.
Ndoa hiyo imetangazwa katika taarifa fupi iliyotolewa na Clarence House.
Taarifa
Taarifa hiyo imesema: "Mwana Mfalme wa Wales, ana furaha ya kutangaza ndoa ya mwanae, Mwana Mfalme William atakayofunga na Bi Catherine Middleton."Harusi itafanyika wakati wa majira ya joto ya mwaka 2011, mjini London. Taarifa zaidi kuhusu harusi hiyo zitatangazwa baadaye.
"Mwana Mfalme William amemfahamisha Malkia na ndugu wengine wa karibu.
"Baada ya kufunga ndoa, wawili hao wataishi kaskazini mwa Wales, ambapo Mwana Mfalme William ataendelea na kazi katika jeshi la Anga la Uingereza Royal
No comments:
Post a Comment