Mwisho wa habari !!
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza lake jipya la mawaziri kukamilisha uundaji wa serikali tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Dr Jakaya Kikwete |
Sura mpya kadhaa zimetajwa ikiwa ni pamoja na Profesa Anna Tibaijuka atakayesimamia wizara ya ardhi na makazi.Profesa Tibaijuka alikuwa mkurugunzi mkuu wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa kabla ya kujiuzulu na kwenda kugombania ubunge jimbo la Muleba Kusini.
Waziri aliyetajwa kinyume na maelezo ya wachambuzi wengi wa kisiasa ni Samuel Sitta, baada ya kuondolewa kiti cha spika wa bunge la Muungano, sasa anakuwa Waziri wa maswala ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wengi wa serikali iliyopitwa wamerejeshwa tena katika majukumu waliyokuwa nayo awali kama vile Bernard Membe atakayeendelea kusimamia mambo ya nje.Mustapha Mkullo anarudi kuongoza wizara ya fedha.
Marekebisho kadhaa ameyataja Rais Kikwete katika uundaji wa baraza lake kuwa idara ya vijana imeondolewa kutoka wizara ya kazi na kuhamishiwa wizara ya habari na michezo.
Wanasiasa kadhaa waliokuwa katika serikali iliyopita wameachwa, baadhi yao ni wasomi maarufu kama Profesa Peter Msola aliyekuwa Sayansi na Teknolojia, Profesa Juma Kapuya aliyekuwa Kazi na Profesa David Mwakyusa aliyekuwa afya, mwingine ni kada wa chama kama John Chiligati aliyeachwa wizara ya ardhi.
Waziri hao wataapishwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Ikulu ya Dar Es Salaam.
Orodha kamili ya mawaziri na manaibu waziri hii hapa chini.
Namba | Ofisi/Wizara | Waziri | Naibu Waziri |
1. | Ofisi ya Rais | 1. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Utawala Bora Mathias Chikawe 2. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu Stephen Wassira | |
2. | Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma | Hawa Ghasia | |
3. | Ofisi ya Makamu wa Rais | 1. Muungano Samia Suluhu 2. Mazingira Dr. Terezya Luoga Hovisa | |
4. | Ofisi ya Waziri Mkuu | 1. Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi 2.Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu | |
5. | Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | George Mkuchika | 1.Aggrey Mwanri 2. Kassim Majaliwa |
6. | Wizara ya Fedha | Mustapha Mkulo | 1. Gregory Teu 2. Pereira Ame Silima |
7. | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | Shamsi Vuai Nahodha | Khamis Kagasheki |
8. | Wizara ya Katiba na Sheria | Celina Kombani | |
9. | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa | Bernard Membe | Mahadhi Juma Mahadhi |
10. | Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa | Dr. Hussein Mwinyi | |
11. | Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi | Dr. Mathayo David Mathayo | Benedict Ole Nangoro |
12. | Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia | Prof. Makame Mnyaa Mbarawa | Charles Kitwanga |
13. | Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi | Prof. Anna Tibaijuka | Goodluck Ole Madeye |
14. | Wizara ya Maliasili na Utalii | Ezekiel Maige | |
15. | Wizara ya Nishati na Madini | William Ngeleja | Adam Kigoma Malima |
16. | Wizara ya Ujenzi | Dr. John Magufuli | Dr. Harrison Mwakyembe |
17. | Wizara ya Uchukuzi | Omari Nundu | Athumani Mfutakamba |
18. | Wizara ya Viwanda na Biashara | Dr. Cyril Chami | Lazaro Nyalandu |
19. | Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi | Dr. Shukuru Kawambwa | Philipo Mulugo |
20. | Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii | Dr. Haji Hussein Mpanda | Dr. Lucy Nkya |
21. | Wizara ya Kazi na Ajira | Gaudensia Kabaka | Makongoro Mahanga |
22. | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto | Sophia Simba | Umi Ali Mwalimu |
23. | Wizara ya Habari, Vijana na Michezo | Emmanuel Nchimbi | Dr. Fenella Mukangara |
24. | Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki | Samuel Sitta | Dr. Abdallah Juma Abdallah |
25. | Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika | Prof. Jumanne Maghembe | Christopher Chiza |
26. | Wizara ya Maji | Prof. Mark Mwandosya | Eng. Gerson Lwinge |
No comments:
Post a Comment