Friday, December 17, 2010

Asamoah Gyan ashinda tuzo ya 2010

Mchezaji nyota wa Ghana na klabu ya Sunderland ya England Asamoah Gyan amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC 2010.
Asamoah
Asamoah Gyan


Mshambuliaji huyo wa Black Stars alishinda kwa kupata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa.
Amepata kura nyingi zaidi ya mchezaji mwenzake wa Ghana Andre 'Dede' Ayew, na pia Yaya Toure na Didier Drogba kutoka Ivory Coast na Samuel Eto'o wa Cameroon.
"Nimefurahi sana, hata siamini," amesema Gyan. "Nawashukuru sana mashabiki wote walionipigia kura." ameongeza.
Gyan
Asamoah
Asamoah Gyan alipatwa na kigugumizi alipopewa taarifa hizo za ushindi kabla ya kusema:
"ilikuwa ni vigumu sana kushinda tuzo hii, hasa kutokana na wachezaji waliotajwa pamoja nami.
"Nawashukuru sana mashabiki wangu wote barani Afrika - hasa familia yangu na mashabiki wa Ghana."

Vichwa vya habari

Gyan amekuawa na mwaka wenye mafanikio makunwa kimatafa, baada ya kuifikisha Ghana katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kushika nafasi ya pili nchini Angola, kwa kufunga mabao matatu kati ya manne ya Ghana na kucheza fainali ya kwanza katika kipindi cha miaka 18.
Katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 aligonga vichwa vya habari kwa kupachika mabao matatu na kuipeleka Black Stars katika robo fainali.
Hata hivyo alitikisa zaidi vichwa vya habari katika mazingira tofauti, baada ya kukosa penati katika mchezo dhidi ya Uruguay ambao ungeipeleka timu ya kwanza kabisa ya Afrika katika nusu fainali.
Gyan
Asamoah Gyan amekuwa na mwaka wenye mafanikio
mamilioni ya mashabiki duniani walitmtiazama mchezaji huyo akitokwa na machozi, ingawa alipata sifa nyingi kwa jinsi alivyojituliza na kufunga bao wakati wa kupiga penati na kuweza kufunga.
Licha ya kupata masikitiko katika Kombe la Dunia, michuano hiyo ilikuza fani yake, kwani aliondoka katika klabu yake ya Rennes ya Ufaransa na kujiunga na Sunderland ya England katika uhamisho ya gharama zaidi kwa klabu hiyo.
Steve
Steve Bruce
"Asamoah amekuwa mchezaji mzuri katika kikosi cha Sunderland," amesema kocha wake Steve Bruce, ambaye amemkabidhi Gyan tuzo hiyo.
"Kama mchezaji wa gharama zaidi katika klabu yetu, kulikuwa na matarajio makubwa sana, na ameweza kufanikisha hilo, vizuri kabisa.
"Ana nguvu, ana kasi na huleta kitu tofauti katika timu.
"Ameweza kucheza vizuri na washambuliaji wengine na amekuwa na mvuto hapa -- wakati wote akitabasamu na mwenye furaha.
"Nimefurahi Asamoah kupata tuzo hii, kwa hakika hii ni hadhi yake." amesema Bruce.
Shughuli ya kumtafuta mchezaji bora wa mwaka 2010 wa BBC ilianza Novemba 15, ambapo mashabiki walipata fursa ya kumchagua mchezaji bora katika orodha ya wachezaji waliochaguliwa na wataalam wa soka kutika nchi 52 za Afrika.

No comments:

Post a Comment